Proverbs 6:29-32

29 aNdivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;
hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.

30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba
kukidhi njaa yake wakati ana njaa.
31 bPamoja na hayo, kama akikamatwa,
lazima alipe mara saba,
ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32 cLakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
Copyright information for SwhNEN